Uhuru Publications Ltd - Gazeti Uhuru, Mzalendo na Burudani

Sunday
Sep 05th
Text size
  • Increase font size
  • Default font size
  • Decrease font size
Home Habari za Mataifa Mbalimbali Europe Cameron akataa kuirejeshea India taji la dhahabu

Cameron akataa kuirejeshea India taji la dhahabu

E-mail Print PDF

NEW DELHI, India

WAZIRI Mkuu wa Uingereza David Cameron amekataa kurejesha taji la malkia lililotengenezwa kwa dhahabu, na kuzawadiwa Malkia Victoria wa Uingereza miaka ya 1800. Malkia Victoria alitawala Uingereza

kuanzia Juni 30, 1837 hadi Januari 22, 1901, ambapo alizawadiwa taji hilo lililopewa jina la Koh-i-noor, kwa maana ya  mlima wenye mwanga. Cameron aliuzwa swali hilo alipokuwa akihojiwa kwenye televisheni, kama Uingereza inaweza kurejesha taji hilo la dhahabu, ambapo alitoa jibu la hapana. Kwa mujibu wa taarifa zilizo tolewa na wasomi wa Kihindu, taji hilo liligunduliwa miaka 700 iliyopita. Taarifa zilisema kuwa taji hilo lilichukuliwa na kampuni ya British East India baada ya mji wa Punjab kutekwa na majeshi ya Uingereza mwaka 1849. Na baadaye taji hilo lilitolewa zawadi kwa Malkia Victoria. Cameron alisema kurejesha taji hilo kutahatarisha vitu vingine vya kiutamaduni vilivyowekwa kwenye makumbusho za Uingereza. Alitoa mfano kuwa Ugiriki imekuwa ikidai kurejeshewa vitu vya kumbukumbu, vilivyochukuliwa nchini humo miaka 200 iliyopita.

 

Kutoka Magazetini

 

TANZANIA ni nchi ya demokrasia yenye kufuata mfumo wa vyama vingi

,  kwa wananchi kuwachangua rais, wabunge na madiwani wanaowataka

 

RAIS wa Zanzibar, Amani Abed Karume

 

 

Umati wa wanaccm wakijimwaga kumlaki mgombea Urais

Umati wa wanaccm wakijimwaga kumlaki mgombea Urais kwa tiketi ya ccm Jk mkoni Mbeya hivi k...

 

MGOMBEA mwenza wa Rais Jakaya Kikwete, Dk. Mohammed Gharib Bilal

, akimnadi kwa wapigakura, mgombea ubunge wa jimbo la Mtwara Vijijini (CCM), Hawa Ghasia k...

 

Mgombea ubunge wa ccm Amos makalla akisalimiana na wananchi jimbo la Mvomero Morogoro. (Picha na Yassin Kayombo).

Magazeti Yetu

Habari za Kitaifa, Kimataifa, Uchumi, Biashara na Michezo kila siku

Habari za Kitaifa, Kimataifa, Uchumi, Biashara na Michezo kila Jumapili

Habari za Michezo, Tamthilia, Makala na Burudani kila Alhamisi

Toa Maoni Yako

Hali ya Kisiasa Tanzania