| Article Index |
|---|
| Simulizi za Mastaa |
| Messi awajaza matumaini wenzake |
| All Pages |
Zidane: Kaka, Benzema watafanikiwa Madrid
MADRID, Hispania
MWANASOKA mkongwe Zinedine Zidane ‘Zizou’ amesema kuwa Kaka na Karim Benzema watapata mafanikio katika klabu ya Real Madrid licha ya kukosa mafanikio yaliyotarajiwa Bernabeu.
Kama Zidane, Kaka alitua katika klabu hiyo msimu huu akitokea AC Milan ya Italia na alitarajiwa angefanya mambo mengi makubwa, lakini ameshindwa kutoa mchango huo.
Karim Benzema, ambaye ni Mfaransa kama alivyo Zizou naye katika klabu hiyo amekuwa na kipindi kibaya na kizuri tangu asajiliwe na Real Madrid akitokea Lyon.
Zizou amesema wachezaji hao watatoa mchango mkubwa katika klabu hiyo baadaye na kamwe hawawezi kukwepa lawama kutoka kwa mashabiki kwani na yeye aliposajiliwa alikumbana nazo.
"Kama ilivyo kawaida hapa Madrid, kuna shutuma. Hivyo ndivyo ilivyo. Baada ya miezi miwili na mimi nilikutana na hali hiyo. Wote ni wachezaji wenye vipaji watafanikiwa," Zidane alisema.








